1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong:kuhamishwa kwa raia wa Asia.

17 Julai 2006

Wakati Israel ikiendeleza mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, nchi za bara la Asia zimekubaliana kwa pamoja kuhamisha raia wao wanaoishi humo hadi pale mashambulizi yatakapokoma.

Australia tayari imeshahamisha raia wake 86, China nayo imewataka raia wake kuihama Lebanon, huku New Zealand naIndonesia ikifanya mipango ya kuwahamisha raia wake.

Waziri wa Mambo ya nje wa Australia Alexander Downer amesema, basi la kwanza lililowabeba raia wake limefanikiwa kwa usalama kuvuka mpaka hadi Syria na hapo kesho pia watafanya jaribio jengine la kuwahamisha.

Wafanyakazi wengine wa Ki- Thailand 25 kati ya 100 wanaofanya kazi Lebanon pia wanahama kwa miguu kutoka katika ardhi ya Beirut kupitia katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon wakilenga kikundi cha wanamgambo wa Hezbollah yamepelekea kuuwawa kwa watu 200 wakiwemo wageni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW