1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hosni Mubarak leo kupandishwa kizimbani

Aboubakary Jumaa Liongo3 Agosti 2011

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak leo anatarajiwa kufikishwa mahakamani takriban miezi sita toka alipolazimishwa na vuguvugu la umma kuondoka madarakani.

Hosni MubarakPicha: AP

Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa vuguvugu hilo la umma, mjini Cairo.Pia Mubarak ambaye alikuwa madarakani kwa kipindi cha takriban miaka 30, anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na kutumia vibaya madaraka yake.

Mapema shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International lilitoa wito wa kufikishwa mahakamani kwa Bwana Mubarak.

Shirika hilo lilisema kuwa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ni tukio la kihistoria nchini Misri kwani linatoa nafasi kwa kiongozi huyo pamoja na utawala wake kuwajibika kwa uhalifu waliyoufanya.

Bwana Mubark amekuwa katika kizuizi cha hospitali kwenye mji wa mapumziko wa Sharm el-Sheikh.Utawala wa Misri umesema kuwa atasafirishwa kwenda kukabiliana na mashtaka yake.Pia na wanawe wawili Alaa na Gamal halikadhalika Waziri wa zamani wa Ulinzi Habib al-Adli nao watapanda kizimbani

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW