MigogoroMashariki ya Kati
Hospitali kusini Gaza zina siku tatu pekee zikiishiwa mafuta
8 Mei 2024Matangazo
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameandika kwenye mtandao wa X kuwa, kufungwa kwa mipaka ya kuingiza misaada ya kiutu kumezuia Umoja wa Mataifa kupeleka mafuta ndani ya Ukanda wa Gaza na kwamba bila huduma hiyo muhimu, shughuli zote za kibinaadamu zitasitishwa.
Tedros ameongeza kuwa Al-Najjar, ambayo ni moja kati ya hospitali tatu zilizoko mjini Rafah, haitoi tena huduma kutokana na oparesheni ya jeshi la Israel mjini humo.
Soma pia: WHO: Gaza bado inakabiliwa na kitisho cha njaa
Licha ya pingamizi kutoka jumuiya ya kimataifa, Israel imetuma vifaru vya kijeshi katika mji wa Rafah na imechukua pia udhibiti wa kivuko cha mpakani cha Kerem Shalom ambacho ni muhimu kwa ajili ya kuingizwa misaada katika Ukanda wa Gaza.