Hospitali kuu ya al-Fashir Sudan yafungwa baada ya shambulio
10 Juni 2024Matangazo
Wahudumu wa kujitolea katika maeneo hayo wanalinyooshea kidole kundi la wanamgambo wa RSF kutokana na shambulizi hilo.
Wapiganaji wa RSF ambao wameudhibiti mji mkuu wa Khartoum na maeneo mengi ya magharibi mwa Sudan pia wanataka kusonga mbele zaidi huku Umoja wa Mataifa ukisema raia wa Sudan wapo katika kitisho cha njaa.
Mji wa al-Fashir ambao upo katika jimbo la Darfur upande wa kaskazini-magharibi mwa Sudan una jumla ya wakazi milioni 1.8 wakijumuishwa na watu waliokimbia makazi yao.
Kwa sasa mji huo umekuwa eneo la mapambano kati ya wanamgambo hao wa RSF na Jeshi la Sudan katika vita vilivyoanza Aprili 2023.