1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya mgombea kiti cha kansela kutoka SPD

Oumilkher Hamidou15 Juni 2009

Matumaini mema ya wana SPD kufuatia mkutano mkuu wa chama

Waziri wa nje Steinemeier akitunukiwa mauwa na mwenyekiti wa SPD MünterferingPicha: AP

Mada mbili kuu zimehanikiza magazetini hii leo;mkutano mkuu wa dharura wa chama cha Social Democratic-SPD na uchaguzi wa rais nchini Iran.

Tuanze na mada ya kwanza ambapo takriban kila uhariri umesifu hotuba ya kusisimua ya waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinemeier .Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:

"Baada ya kipindi kigumu cha wiki kadhaa,SPD kimeanza upya kuvuta pumzi.Mkutano wa kilele ulikua kama njia mojawapo ya kujizindua,ulikua kama tiba baada ya zilzala ya uchaguzi wa bunge la Ulaya pamoja pia na matokeo mabaya ya maoni ya umma.Angalao waatu wameanza kupumua hivi sasa,badala ya kuduwaa na kukata tamaa.Alikua mgombea kiti cha kansela Franz-Walter Steinemeier aliyepindua hali ya mambo kwa kutoa hotuba kali kabisa -ya kwanza ya aina yake tangu alipoteuliwa kugombea wadhifa huo.Waziri wa mambo ya nchi za nje amedhihirisha kwamba nayeye pia ameshajifunza.Kinyume na hali namna ilivyokua wiki za nyuma,safari hii Steinemeier ametungumzia shabaha za kisiasa za chama cha SPD na sio makosa ya wapinzani wao wa kisiasa."

"Sifa zimetolewa pia na gazeti la Die Welt linaloandika:

"Frank -Walter Steinemeier amefanikiwa kukipa moyo chama kilichokua kimekata tamaa.Amekidhi matarajio ya wote waliokua wakiisubiri kwa hamu hotuba yake.Badala ya kutoa maneno makali makali,Steinmeier amechagua kukirejesha upya chama cha SPD katika siasa za mrengo wa kati.Kwa kutambua makosa yaliyotokea katika kutatuliwa mgogoro wa kampuni la magari la Opel na kampuni la Arcandor,ameonyesha hali ya kujiamini.Na akahakikisha SPD iko upande wa wafanyakazi wa Opel na wale wa Karstadt.Mgombea kiti cha kansela amekwenda mbali zaidi na kujitambulisha na "sera mpya za mrengo wa kati za mwaka 1998-" na hapo hata kansela wa zamani Gerhard Schröder alishangiria".

Mada ya pili magazetini ni kuhusu uchaguzi wa rais nchini Iran.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:

"Pengine ni kweli kwamba Ahmedinedjad amejipatia wingi wa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi.Lakini kishindo cha mikururo ya wafuasi wa Mussawi,kimeifanya serikali pengine isithubutu kuruhusu duru ya pili.Ndio maana wameamua kutangaza matokeo bandia ,kumaliza udhia.Uchaguzi ulikua kiini macho tuu na kutaka kuiga mitindo ya nchi za kidemokrasi kwa kutangaza matokeo ya mwanzo.Lakini masharti ya kuwepo utaratibu wa kuaminika kama huo yanakosekana nchini Iran.Hakuna utaratibu wa kuaminika wa kukusanya maoni ya umma,seuze maoni kuhusiana na kutishwa duru ya pili ya uchaguzi au mtambo wa komputor kurahisisha mambo hayo.Kilichokuwepo lakini ni vurugu na hali ya kila aina ya kubabaisha."


Mwandishi: Hamidou, Oumilkher

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW