HOUSTON : Kimbunga Rita changuruma Marekani
22 Septemba 2005Nchini Marekani Kimbunga Rita leo kimegeuka kuwa dhoruba kubwa ya upepo unaokimbia kilomita 265 kwa saa wakati ukilikumba eneo zima la Ghuba ya Mexico na kuwalazimisha wafanyakazi wa vituo vya uchimbaji wa mafuta baharini kutelekeza vituo vyao na mamia na maelfu ya watu kulikimbia eneo la mwambao la Texas.
Ikiwa bado chini ya shutuma kutokana na jinsi ilivyoshughilia athari za Kimbunga Katrina serikali ya Marekani imewaagiza watu kuondoka kwenye bandari ya Texas ya Galveston na sehemu za mji wa Corpus Christi.Watu wachache walioko kwenye maeneo ya New Orleans na Loussiana pia wametakiwa waondoke kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi wiki nne.
Zaidi ya watu milioni moja wameamuriwa waondoke.
Ghuba ya Mwambao nchini Marekani bado haikurudi katika hali yake ya kwaida kutokana na kukumbwa na Kimbunga cha Katrina wiki tatu zilizopita ambacho kimesababisha kupotea kwa maisha ya watu zaidi ya 1,000.