1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Houthi waishambulia meli ya China kwenye Bahari ya Shamu

24 Machi 2024

Vikosi vya Marekani vimesema wanamgambo wa Houthi wanaosaidiwa na Iran wameishambulia meli ya mafuta ya China katika Bahari ya Shamu jana Jumamosi.

Ghuba ya Aden | Meli ya Rubymar ikizama baada ya kushambuliwa
Machi 7, 2024: Picha inaonyesha moja ya meli ya mizigo iliyoshambuliwa na waasi wa Houthi katika Bahari ya Shamu ikiwa inazama. Picha: Khaled Ziad/AFP/Getty Images

Kamandi kuu ya kijeshi ya Marekani, CENTCOM imesema vikosi vya Houthi vilifyatulia makombora manne meli hiyo ya M/V Huang Pu asubuhi ya jana. Kwenye majira ya saa 4.25 za jioni za eneo hilo, waligundua kombora jingine lililofyatuliwa kuelekea meli hiyo.

CENTCOM imesema meli hiyo imeharibiwa kiasi na walifanikiwa kuuzima moto uliowaka ndani ya meli baada ya nusu saa. Hakukua na majeruhi wala kifo na meli hiyo iliendelea na safari.

Wanamgambo hao wameapa kushambulia meli zinazopita kwenye Bahari ya Shamu na zenye mahusiano na Israel, ingawa meli nyingi zilizoshambuliwa hadi sasa hazina mahusiano na taifa hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW