1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Congo haijachunguza mauaji ya watu wa Iyeke

9 Februari 2022

Shirika la Human Rights Watch limesema serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeshindwa kufanya uchunguzi kamili wa mauaji ya karibu watu 66 wa kabila la Iyeke katika wilaya ya Bianga kwenye jimbo la Monkoto

Human Rights Watch | Logo
Picha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Bunge la kitaifa la Congo liliipigia kura mwaka jana sheria ambayo kwa mara ya kwanza ingelinda na kukuza haki za watu wa jamii za Kiasili, lakini mswada huo bado umekwama kwenye baraza la seneti.

Kuanzia Februari mosi hadi tatu mwaka wa 2021, mamia ya washambuliaji wa kabila la Nkundo waliwauwa wanakiji wa kabila la Iyeke, wakiwemo watoto 40, wanaume 22 na wanawake 4, na kuwajeruhi wengine wengi katika vijiji vinane. Wavamizi hao pia walichoma moto Zaidi ya nyumba 1,000 pamoja na shule, makanisa, na vituo vya afya kwa mujibu wa manusura, mashuhuda, makundi ya kiraia na maafisa wa mkoa.

Maafisa awali walianzisha uchunguzi lakini hawakwenda katika maeneo yalioathirika kwa ajili ya upelelezi. Mwaka mmoja umepita na hakuna hata mmoja aliyeshitakiwa kwa mauaji hayo, ambayo hata hayajaripotiwa sana na vyombo vya Habari. Watu wawili waslishitakiwa na kufutiwa kesi ya makosa madogo na kesi ikafungwa.

Mtafiti mwandamizi wa Human Rights Watch Thomas Fessy amesema kimya hicho kuhusiana na mauaji hayo ya kikatili ya wanakijiji wa Iyeke na kukosekana kwa uwabikaji vinaonyesha ugabuzi wa muda mrefu dhidi ya watu wa asili nchini Congo.

Uchunguzi wa HRW ulitokana na ziara ya utafiti ya Oktoba 2021 katika mkoa wa magharibi wa Monkoto. Shirika hilo liliwahoji watu 44, wakiwemo manusura wa Iyeke na mashuhuda wa mashambulizi hayo, wanakijiji wa Nkundo, maafisa wa mahakama, wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wabunge, maafisa wa mkoa na maafisa wa jeshi.

Mashambulizi hayo yalisababisha Zaidi ya watu 8,000 wa kabila la Iyeke kukimbilia porini, Kambako waliishi kwa karibu miezi sita. Maafisa wa mkoa na wabunge walitoa msaada wa kifedha kufuatia mashambulizi hayo, ikiwemo malipo kadhaa kwa ajili ya waliopoteza Maisha. HRW inasema msaada uliotolewa haukutosha kugharamia hasara iliyopatikana.

Mauaji hayo yalitokea wakati wa ongezeko la mvutano kati ya jamii za Nkundo na Iyeke kufuatia mauaji ambayo hayajatatuliwa ya mfanyakazi mmoja wa Iyeke mnamo Desemba 2020, karibu na Kijiji cha Bondjindo. Mwili wake ulipatikana ukiwa umekatwa katwa katika shamba moja linalomilikiwa mtu wa jamii ya Nkundo. Wanakijiji wa Iyeke wakaishuku familia ya mmiliki wa shamba hilo na kupora na kuyachoma makazi yao kulipiza kisasi.

Jamii hizo mbili zinaishi katika vijiji tofauti lakini vilivyo jirani kando ya Mbuga ya Kitaifa ya Salonga, katika mkoa wa Tshuapa. Mivutano ya muda mrefu kati ya makundi hayo mawili huhusisha upatikanaji wa mashamba na ajira ya utumwa.

Chanzo: HRW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW