HRW: Kenya ichunguze mauaji ya waandamanaji
21 Juni 2016Matangazo
Human Rights Watch imetoa ripoti yake ya utafiti inayolituhumu jeshi la polisi nchini Kenya kutumia nguvu ya ziada kuwatawanya waandamanaji katika mkoa wa Nyanza magharibi mwa nchini hiyo mnamo Mei 23 na Juni 6 2016 ambapo watu watano waliuawa na wengine 60 kujeruhiwa. Maandamano hayo yaliitishwa na muungano wa upinzani nchini Kenya, CORD, unaotaka kuvunjwa kwa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi ya nchi hiyo, IEBC. Isaac Gamba amezungumza na Otsieno Namwaya ambaye ni mtafiti wa shirika hilo kanda ya Afrika kutaka kujua walichobaini katika utafiti huo.