1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Makaburi ya halaiki yagunduliwa Burkina Faso

8 Julai 2020

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza habari ya kugunduliwa makaburi ya umati yenye maiti 180 kaskazini mwa Burkina Faso.

Massengrab im Sudan entdeckt
Picha: Afp

Shirika hilo linawatuhumu maafisa wa usalama wa Burkina Faso kuwa wamehusika na mauaji hayo ya mamia ya watu waliowakamata katika operesheni zao dhidi ya makundi ya kigaidi. Kufuatia tuhuma hizo Serikali inasema itaendesha uchunguzi.

Ripoti ya HRW inasema mauaji hayo ya raia yaliwalenga hasa wanaume wa kabila la Peul na walizikwa kati  ya Aprili na Mei. Maiti nyingi zilikuwab zimefunikwa macho na kufungwa mikono watu hao waliuliwa kwa kupigwa risasi kichwani yameandikwa kwenye ripoti hiyo ikimtaja mmoja wa viongozi wa jamii hizo kwenye mji huo.

Sio mara ya kwanza serikali kutuhumiwa kuhusika kwa mauwaji ya kukusudia katika vita vyake dhidi ya makundi ya kidaidi ya Al-Qaida na lile linalojiita dola la kiislamu ISIS.

Picha: DW/D. van der Linde

Toka mwaka 2015, Burkina Faso inakabiliana na uasi wa kigaidi uliosabisha vifo vya mamia ya raia na kuwalazimisha wengine wapatao milioni moja kuyahama makaazi yao. Machafuko hayo yanaathiri pia nchi jirani za Niger na Mali.

Wito wa kufanyika uchunguzi watolewa

Corinne Dufka, Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika eneo la Sahel, Afrika Magharibi ameitaka serikali ya Ougadougou kuchunguza mauaji hayo na kuwafikisha mbele ya sheria waliotenda jinai hiyo, kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Hata hivyo, Moumina Cheriff Sy, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema serikali itachunguza jinai hiyo na kueleza kwamba yumkini mauaji hayo yalifanywa na wanachama wa magenge ya kigaidi waliovalia magwanda ya kijeshi waliyoyaiba.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yamelezea kwamba serikali haijapiga hatua kubwa katika kuendesha uchunguzi kuhusu ukeukaji wa haki za binadamu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika.

Kwenye mkutano wa kilele wa Juni 30 ,kuhusu usalama wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Sahel waliwambia viongozi wa Burfina Faso kwamba afisa yeyote wa jeshi atakayehusika na ukeukaji wa haki za binadamu atapewa adhabu kali.

Mwandishi : Saleh Mwanamilongo

Mhariri : Zaainab Aziz