1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Mshikamano umeimarika dhidi ya ukiukaji duniani

12 Januari 2023

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema upinzani mkubwa dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeonyesha mshikamano wa pamoja kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu.

Human Rights Watch | Logo
Picha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Kuna dalili kwamba nguvu inahamia kwa raia nchini Iran wanaoandamana kudhihirisha kutoridhika kwao, na pia nchini China na kwingineko. 

Katika ripoti yake ya kila mwaka ya dunia kuhusu hali ya haki za binaadamu katika nchi na maeneo 100, shirika la Human Rights Watch limesema ``mgogoro wa haki za binadamu'' uliibuka mwaka wa 2022, lakini mwaka huo pia uliwasilisha fursa mpya za kuimarisha ulinzi dhidi ya ukiukaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Human Rights Watch, Tirana Hassan, ametaja Afghanistan, Sudan Kusini na uhamasishaji wa ulimwengu kuhusu Ukraine inakumbusha juu ya uwezo usio wa kawaida wakati serikali zinapotambua wajibu wao wa haki za binadamu duniani kote, katika utangulizi wa ripoti hiyo yenye kurasa 712.

Kufuatia uvamizi wa Urusi kwa Ukraine, kundi kubwa la mataifa liliwekewa vikwazo vingi wakati wa kuisaidia Kyiv, na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa Jinai walifungua uchunguzi juu ya unyanyasaji.

Hassan amesema kwamba nchi sasa zinahitaji kujiuliza ni nini kingetokea ikiwa walichukua hatua kama hizo baada ya Urusi kuivamia Crimea mwaka 2014, au kutumia waliyojifunza nchini Ethiopia, ambapo miaka miwili ya migogoro ya silaha imechangia moja ya mgogoro mbaya zaidi wa kibinaadamu duniani.

Nguvu ya umma

Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Shirika hilo lenye makao yake mjini New York liliangazia maandamano yaliyoibuka nchini Iran katikati mwa Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini akiwa chini ya ulinzi wa polisi jamii, pamoja na maandamano huko Sri Lanka ambayo yalilazimisha serikali ya Rais Gotabaya Rajapaksa kujiuzulu, na kuchaguliwa kidemokrasia kwa rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva dhidi ya mpinzani wake Jair Bolsonaro.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ripoti hiyo mjini Jakarta, Mkurugenzi wa Asia wa shirika la Human Rights Watch Elaine Pearson amesema watu wanaonesha ujasiri mara kwa mara kwa kuchukua hatua za hatari, kuandamana hata katika maeneo kama Afghanistan na China ili wasimamie haki zao.

Aidha Shirika la Human Rights Watch limesema Umoja wa Mataifa na mataifa mengine yaliongeza kuzingatia kuhusu suala la jamii ya waislamu wa Uyghur na Ururuki katika mkoa wa Xinjiang nchini China na kuiweka Beijing katika uangalizi huku maandamano yaliyopinga mkakati wa serikali wa kuondoa kabisa Uviko- 19 ulijumuisha ukosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Xi Jinping.

Wakati serikali nyingi za Magharibi zikiachana na  China kwenye biashara na kuelekea India, Pearson aliwaonya wasimpuuze rekodi ya haki za binaadam ya waziri mkuu wa India Narendra Modi.

 

//AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW