HRW: Yaitaka Lebanon kumuachia huru Hannibal Gadafi.
16 Januari 2024Matangazo
Human Rights Watch imesema Hannibal Gadafi amezuiliwa kwa kile ilichosema ni "mashtaka ya uwongo" kwa muda wa miaka minane.
Mnamo mwaka 2015, Lebanon ilimkamata na kumtuhumu Hannibal Gadafi, anayejulikana kwa kuishi maisha ya anasa, kwa kuficha habari juu ya kupotea kwa kiongozi wa Kishia Imam Mussa Sadr, mwaka 1978.
Human Rights imeeleza kuwa, Hannibal Gadafi alikuwa na umri wa miaka miwili tu wakati kiongozi huyo alipotoweka, na imeishtumu Lebanon kwa kumuweka kizuizini katika kile kinachoonekana kuwa ni mashtaka ya uwongo.
Sadr ambaye ni mwanzilishi wa vuguvugu la Amal, ambalo sasa ni mshirika mkuu wa kundi la Hezbollah - alitoweka wakati alipofanya ziara nchini Libya akiwa pamoja na msaidizi wake na mwandishi mmoja wa habari.