1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yataka wahusika waliosalia wa mauaji ya Rwanda wakamatwe

2 Aprili 2024

Shirika la Human Rights Watch limesema kuna haja ya kuwasaka wahusika wakuu waliosalia wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda, siku tano kabla ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kufanyike ukatili huo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Paul Kagame wa Rwanda.Picha: Halil Sagirkaya/Anadolu/picture alliance

Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binaadamu lilisema katika taarifa yake ya siku ya Jumanne (Aprili 2) kwamba ingawa idadi kubwa ya watu waliohusika namauaji hayo ya kimbari, ikiwa ni pamoja na maafisa wa zamani wa ngazi za juu wa serikali na watu wengine muhimu, tayari wamefikishwa mahakamani, lakini kuna umuhimu wa kuendelea na azma ya kutenda haki.

Soma zaidi: HRW yaishutumu Rwanda kwa mauaji ya wakosoaji nje ya nchi

Shirika hilo limeongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, wahusika kadhaa wa mauaji hayo wamekufa, huku mmoja wao akitangazwa kuwa dhaifu kiafya na hafai kujibu mashtaka yanayomkabili.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, mauaji ya siku 100 ya kimbari nchini Rwanda mnamo mwaka 1994 yalisababisha vifo vya karibu watu 800,000, wengi wao wakiwa Watutsi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW