HRW yawataka wabunge wa Gambia kutoruhusu ukeketaji
19 Aprili 2024Matangazo
Shirika hilo la kimataifa limesema muswaada huo unasababisha mashaka makubwa katika suala la haki za wanawake.
Ukeketaji ni kitendo kilichopigwa marufuku kisheria katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi tangu mwaka 2015, lakini mnamo mwezi March wabunge walipiga kura ya kuupeleka muswaada huo wenye utata kwenye kamati maalum ya kuutathmini kabla ya bunge kuchukua hatua ya mwisho ya kuupigia kura.
Soma zaidi: Kenya: Kampeni ya kukabiliana na ukeketaji wazinduliwa
Shirika la Human Rights Watch limesema, ikiwa bunge litaidhinisha muswaada huo uliofanyiwa marekebisho mwezi Juni, basi Gambia itakuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu tena ukeketaji.