1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

HRW:Mradi wa bomba la mafuta Uganda ni janga kwa sayari.

Hawa Bihoga
10 Julai 2023

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limehimiza kusitishwa kwa mradi mkubwa wa mafuta wa Afrika Mashariki, unaoongozwa na kampuni kubwa ya Ufaransa ya TotalEnergies, kutokana na kutozingatia haki.

Human Rights Watch Joe Stork
Picha: AFIN HAMED/AFP/Getty Images

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limehimiza kusitishwa kwa mradi mkubwa wa mafuta wa Afrika Mashariki unaoongozwa na kampuni kubwa ya Ufaransa ya TotalEnergies, na kuonya juu ya athari mbaya kwa mazingira na jamii hasa maeneo ambayo bomba hilo linapita.

Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki limekuwa likipata upinzani mkali kutoka kwa wanaharakati wa haki na mashirika ya mazingira, na kukabiliwa na hatua za kisheria nchini Ufaransa na ukosoaji katika Bunge la Ulaya.

Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika hilo la Kimataifa la kutetea haki za binadamu unasema mradi huo mkubwa utaharibu kwa njia isiyoweza kurekebishwa mifumo dhahifu ya  ikolojia.

Soma pia:Mbunge wa Ujerumani aukosoa mradi wa EACOP

Watafiti walifanya mahojiano na zaidi ya kaya  90 mwezi Machi na Aprili mwaka huu, ikiwa ni pamoja na familia 75 zilizohamishwa.

Wengi kati yao walisema walipokea malipo ya fidia kiduchu kwa kuchelewa na wengine walishinikizwa kuuza ardhi zao kwa haraka.

"Mradi huo umekuwa janga kwa maelfu ya familia." Alisema Felix Horne, mtafiti mkuu wa mazingira katika shirika hilo.

"Walilazimishwa kuuza ardhi zao walizotumia kulima kwa ajili ya chakula na kuuza mazao kwa ajili ya kuzikimu familia." Aliongeza Horne.

Wananchi:Tulilipwa fidia isokidhi

Wakulima waliiambia Human Rights Watch kwamba,  iliwabidi kusubiri kwa miaka kadhaa kulipwa fidia zao.

Wakati wakisubiri malipo yao baadhi ya wanaharakati wakifungua kesi 37ambapo watoto walidaiwa kulazimika kuacha shule kutokana na  familia zao kushindwa kulipa ada.

Soma pia:Bomba la mafuta la Afrika Mashariki lakabiliwa na mtikisiko

Baadhi walitia saini mikataba ya fidia ilioandikwa kwa Kiingereza, lugha ambayo hawaijui, huku wengine waliwaambia watafiti kwamba "uwepo wa maafisa wa serikali na usalama kwenye mikutano ya hadhara ulichangia hali ya vitisho"

Horne amesisistiza katika ripoti hiyo inayoonesha kuendelea kwa mradi huo kutasababisha takriban watu 100,000 kuhamishwa kwamba, bomba hilo halipaswi kuendelea na ujenzi wake kwa kuwa ni "janga kubwa" kwa sayari.

Museven aapa kuendelea na mradi huo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameapa kuendelea na mradi huo licha ya Bunge la Ulaya kutaka ucheleweshwe kutokana na "ukiukaji wa haki".

Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: picture alliance/dpa/Russian Foreign Ministry

Mashirika matano ya misaada kutoka Uganda na Ufaransa pamoja na Waganda 26 waliishtaki kampuni ya Total Energies mjini Paris mwezi uliopita kwa malipo ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika miradi yake miwili mikubwa nchini humo, ikiwa ni pamoja na mradi huo wa bomba la mafuta ghafi Afrika mashariki.

Katika barua ya Juni 15 ilioelekwazwa kwa Human Rights Watch, Total Energies ilisema imetoa fidia ya haki na "itaendelea kuzingatia kwa makini kuheshimu haki za jamii husika".

Soma pia:Museveni aapa kuendeleza mradi wa mafuta licha ya upinzani wa Bunge la Ulaya

Hata hivyo rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akiusifu hadharani mradi huo na kuutaja  kama uimarishaji mkubwa wa kiuchumi kwa nchi hiyo isiyo na bahari, ambapo watu wengi wanaishi katika umaskini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW