1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huduma ya afya: Ujerumani yajaribu kuzuwia utapeli

23 Julai 2023

Mashirika ya uwekezaji ya kimataifa yananunua kliniki nchini Ujerumani, hali inayochochea hofu ya wagonjwa kuhusu matibabu ya gharama kubwa lakini yasiyo ya laazima. Lakini wengine wanasema uwekezaji unaleta maboresho.

Symbolbild | Schönheit-Operationen
Upasuaji wa macho ni kati ya matibabu yenye faida kubwa.Picha: A. Noor/BSIP/picture alliance

Nchini Ujerumani, wagonjwa wanazidi kuwa na wasiwasi kwamba wanazungumziwa kuhusu matibabu yasiyo ya lazima na madaktari wao huku vikundi vya uwekezaji wa kigeni vikinunua kliniki zaidi na zaidi. Hii inatokea hasa kwa zile zinazotoa huduma za gharama kubwa zaidi ambazo hazilipiwi na bima, kama vile kliniki za macho, kliniki za radiolojia na madaktari wa meno.

Utafiti uliochapishwa mwezi wa Mei na shirika la utafiti wa kifedha la Finanzwende uligundua kuwa makampuni ya kibinafsi yalinunua kliniki 174 za madaktari wa Ujerumani mwaka 2022, kutoka 140 mwaka 2021 na mbili pekee mwaka 2010. Na, kulingana na utafiti wa shirika la utangazaji la umma NDR, makampuni kama hayo sasa yanamiliki mamia ya kliniki kote Ujerumani, kiasi kwamba kampuni moja inahodhi kliniki hizo katika baadhi ya majimbo na miji.

Suala hilo liliibuka kwenye rada ya serikali ya Ujerumani mwaka jana. "Ninasimamisha wawekezaji kununua kliniki za udaktari kwa uroho wa faida," waziri wa afya, msosho demorkat Karl Lauterbach alitangaza katika mazujgumzo na gazeti la Bild am Sonntag mwezi Desemba, kabla ya kuahidi kuwasilisha mswada "wa kukomesha nzige hawa kuingia katika shughuli za matibabu."

Wawekezaji hutoa vifaa vya kisasa kwa kliniki za madaktari.Picha: Jörg Carstensen/dpa/picture alliance

Pesa kwa wagonjwa

Horst Helbig, msemaji wa Jumuiya ya matabibu wa macho, DOG, na mkurugenzi wa kliniki ya macho katika jiji la Regensburg, alisema kliniki zinazomilikiwa na wawekezaji zinalenga kupata faida. "Madhumuni ya kikundi cha uwekezaji ni kupata faida kwa asilimia 100 - hawataki kitu kingine chochote, na, mwisho wa siku, hawaruhusiwi kufanya kitu kingine chochote," alisema. "Bila shaka, kliniki zinazomilikiwa na daktari mmoja pia zinahitaji kupata pesa, lakini lengo lake kuu ni kutoa huduma ya matibabu."

Utafiti wa 2022 wa taasisi ya utafiti ya IGES ulionekana kuunga mkono hilo, na kugundua kuwa kliniki zinazomilikiwa na wawekezaji zilichukua ada zaidi ya asilimia 10.4 kuliko kliniki zinazomilikiwa na madaktari binafsi. Lakini baadhi ya vyama vya huduma za matibabu, kama vile BBMV, ambacho kinawakilisha waendeshaji wa vituo vya huduma za matibabu (MVZ), vinapinga hitimisho kwamba MVZ hazijitegemei kiafya.

Soma pia:Ujerumani yatumai kuidhibiti Omicron, lakini waziri aonya dhidi ya kulegeza vikwazo 

Ujerumani ina mfumo wa huduma za afya wa ngazi mbili unaofadhiliwa na michango ya wafanyakazi na waajiri kwa makampuni ya bima za afya. Bima ya afya ni ya lazima kwawatu wote, na watoaji wa bima, ambao wanashughulikia karibu asilimia 90 ya watu, hawaruhusiwi kukataa bima ya mtu yeyote. Takriban asilimia 10 ya watu huchagua bima ya kibinafsi, ambayo mara nyingi hutoa huduma zaidi. Kwa ujumla, mfumo wa afya wa Ujerumani una thamani ya euro bilioni mia kadhaa kwa mwaka.

Helbig alisema amegundua mwelekeo wa kliniki za madktari zinazomilikiwa na  wawekezaji kuwakataa wagonjwa walio na bima ya umma ili kujikita kwa wale ambao watawapatia faida. "Wagonjwa wengine wana faida kubwa, wengine wanagharimu pesa, na tulichogundua ni kwamba wagonjwa wengi ambao hawawezi kutibiwa kwa faida wanahamishiwa katika hospitali za umma," aliiambia DW.

Waziri wa Afya Karl Lauterbach aliapa kusitisha wawekezaji kununua kliniki za madaktari zinazoendeshwa na uroho wa faida.Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Hii inaonekana hasa katika kliniki za macho kama vile ya Helbig, alisema, ambapo kuna tofauti kubwa za bei kati ya matibabu, ambayo baadhi hayalipiwi na bima. "Kinacholipwa vizuri ni upasuaji wa mtoto wa jicho, wakati aina yoyote ya utaratibu wa dharura hailipiwi vizuri," Helbig alisema.

Ruwaza hatari ya kibiashara

Vivutio vya fedha za hisa za kibinafsi ni dhahiri: Finanzwende ilikokotoa kuwa wanaweza kutarajia kupata hadi asilimia 20 ya faida kwenye uwekezaji wao - lakini ikiwa tu watanunua kliniki za kutosha. Mtafiti wa Finanzwende Aurora Li alisema mtindo wa biashara wa fedha za hisa binafsi unategemea kuunganisha kliniki kadhaa na kufanya marekebisho hatari ya uendeshaji kwake - kwa sehemu kupitia mikopo - ili waweze kuziuza kwa faida baadaye.

"Fokasi sio faida ya uendeshaji, lakini kwenye mtiririko thabiti wa pesa," Li aliiambia DW. "Kwa hivyo ikiwa kampuni inaweza kudumisha mzunguko wa fedha wa kutosha kupitia shinikizo kwa madaktari kuuza matibabu ya faida, na kwa kutumia uwekezaji mdogo lakini mikopo zaidi, basi inaweza kuifanya kampuni kuwa na faida kwa wawekezaji wengine wa kifedha. Na unaweza tu kuunda mzunguko mkubwa wa pesa ikiwa una ofisi nyingi za madaktari."

"Inatia wasiwasi sana hasa wakati wagonjwa wanapokuwa hawawezi kuwa na uhakika kwamba matibabu yao hayaathiriwi na matarajio ya faida," aliongeza.

Muswada ulioahidiwa na waziri wa afya Lauterbach bado haujatimia, lakini baadhi ya vyama vya matibabu tayari vimekosoa chaguo lake la maneno kama "nzige." BBMV ilisema data za serikali zinaonyesha hakuna ushahidi wa takwimu kwamba matibabu katika kliniki zinazomilikiwa na mfuko wa uwekezaji ya ubaya wowote.

Madaktari walioajiriwa katika vituo vya huduma za matibabu walichapisha barua mnamo Mei wakipinga kwa hasira maoni la Lauterbach kwamba uhuru wao unaweza kutiliwa shaka. "Kama madaktari walioajiriwa, tunafanya taaluma yetu kwa shauku na kujitolea sawa kwa mgonjwa kama wenzetu kutoka kliniki za kibinafsi ... au hospitalini. Kwa bahati mbaya, tunaona kazi yetu ... inadharauliwa hadharani."

Ongezeko la maambukizi ya COVID-19 Ujerumani

02:57

This browser does not support the video element.

Lengo la faida

BBMV inabainisha kuwa kliniki zinazomilikiwa na madaktari binafsi zina msukumo sawa wa kupata faida. Hiyo ni kweli kwa kiasi fulani, anasema Helbig. "Kwa hakika kuna madaktari wengi wanaofanya kazi katika kliniki inayomilikiwa na kundi la uwekezaji ambao hawakubali kushinikizwa," alisema. "Na bila shaka, kuna madaktari ambao wana kliniki moja ambayo matibabu sio kipaumbele kwao." Lakini shinikizo, alisisitiza, lilikuwa kubwa zaidi kwa kliniki zinazomilikiwa na wawekezaji.

Roland Stahl, msemaji wa KBV, chama ambacho kinawakilisha maslahi ya wamiliki w akliniki wa Ujerumani, alichukua msimamo wa upatanishi zaidi. "Sio kila mwekezaji ni nzige," aliiambia DW. Lakini ni tofauti, aliongeza, wakati vikundi vya uwekezaji vinaponunua kliniki katika maeneo moja ili kuunda mazingira ya kuhodhi.

"Kwa kweli, hilo linahitaji kutazamwa, lakini uwekezaji wa mtaji unaweza kuwa mzuri," alisema. "Kwa sababu wakati mwingine hurahisisha ununuzi wa vifaa vya matibabu vinavyohitaji mtaji mkubwa, kama vile skana za MRI, kwa mfano."

Helbig pia hapingani na wazo la kuunganisha kliniki kimsingi, kwa sehemu kutokana na ukweli kliniki  zikochini ya shinikizo nyingi tofauti za kiuchumi kiasi kwamba mfumo hauwezi kutekelezeka katika hali yake ya sasa. Madaktari wachache vijana, alisema, wako tayari kutafuta uwekezaji na kujiweka katika wiki za masaa 60 zinazohitajika kuanzisha kliniki zao wenyewe.

"Ni vigumu sana kufanya hivyo peke yako tena," Helbig alieleza. "Ina maana kushiriki yote hayo, kwa hivyo mabadiliko fulani ni muhimu."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW