1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huduma za ndege zarejea baada ya hitilafu ya kimtandao

20 Julai 2024

Mashirika ya ndege yameanza kurejea kufanya shughuli kama kawaida baada ya kukumbwa na hitilafu kubwa ya kimtandao ambayo ilipelekea msukosuko kwa huduma za usafiri wa kimataifa, benki na matangazo ya televeisheni

Uwanja wa ndege wa London, Uingereza
Idadi kubwa ya abiria wa ndege wakiwa wanasubiri matangazo ya ndege zao baada ya hitilafu ya mifumo ya kompyuta na mtandao Picha: Joe Giddens/AP/dpa/picture alliance

Mashirika ya ndege yameanza kurejea mtandaoni hatua kwa hatua mapema Jumamosi baada ya kukumbwa na hitilafu kubwa ya kimtandao ambayo ilipelekea msukosuko mkubwa kwa watoa huduma za usafiri wa kimataifa, benki na hata matangazo ya televeisheni.

Hapo jana umati mkubwa wa abiria ulikuwa umekusanyika katika viwanja mbalimbali vya ndege kusubiri habari za lini ndege zao zilizokuwa zimesitisha huduma zitarejea katika mfumo wa kawaida.

Soma zaidi.Hitilafu ya mtandao yaripotiwa maeneo kadhaa duniani 

Mashirika mengi ya ndege kuanzia Ulaya, Marekani hadi kote barani Asia yameripoti kuwa kwa sasa yanaendelea na shughuli zao ingawa bado katika baadhi ya viwanja,  ndege zinaripotiwa kuwa zitachelewa.

Waatalam wa teknolojia wanasema hitilafu hii ya kimtandao ni kubwa kuwahi kutokea kwa miaka ya karibuni na kwamba itaingia katika historia kwa kuleta athari kubwa katika maeneo mengi duniani.

  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW