Huenda Champions League ikafanyiwa mabadiliko
25 Machi 2016Hayo ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza na Uhispania. Gazeti Uingereza la The Guardian likinuu duru za klabu moja kuu ya Premier League, limesema mabadiliko hayo yataunda kile kitakachokuwa ni ligi mbili ndogo. Gazeti la Mundo Deportivo la Uhispania pia lilizungumzia makundi mawili ya timu nane.
Chama cha mashirikisho la kandanda Ulaya – UEFA kimesema hakuna mapendekezo imara kwa sasa kwa sababu mabadiliko hayawezi kutekelezwa hadi mwanzoni mwa msimu wa 2018 na 19 kutokana na sababu za mikataba. Uamuzi wa kamati kuu ya UEFA unatarajiwa kufanywa mwishoni mwa mwaka huu.
Schweinsteiger huenda akacheza Euro 2016
Nahodha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger ana nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha dimba la EURO 2016 licha ya kupata jeraha. Hayo ni kwa mujibu wa meneja wa timu Oliver Bierhoff.
Kiungo huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka 31 alipata jeraha la mshipa wa goti wakati akiwa mazoezini Jumatano kabla ya michuano ya kirafiki ya England na Italia. Atakuwa mkekani kwa wiki kadhaa na Bierhoff anaamini kuwa atarejea kabla ya kuanza dimba la Uefa Euro 2016 nchini Ufaransa litakaloanza Mei 30 hadi Julai 10.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu