Huenda dhahabu kaskazini mwa Mali ikawanufaisha magaidi
14 Februari 2020Matangazo
Kuna hofu kwamba huenda madini hayo yakaunufaisha sio tu uchumi wa eneo hilo bali hata wanamgambo wa Kiislamu.
Muungano wa waasi wa Tuareg wanaojulikana kama CMA wanalidhibiti eneo la Kidal na viongozi wake ndio wanaosimamia mpango huo wa dhahabu.
Baadhi ya wanachama wa CMA wanaaminika kuwa na mahusiano ya karibu na kundi la JNIM ambalo ni mshirika wa al-Qaida katika eneo hilo.
Maafisa wa CMA wamekataa kuzungumzia uwepo wa wapiganaji walio na uhusiano na al-Qaida miongoni mwao.
Wakaazi pia wanahofia kuzungumzia suala hilo wakisema kundi hilo la magaidi lina maafisa wa kijasusi katika kila sehemu mjini humo.