Huenda UAE isishiriki katika juhudi za kuleta utulivu Gaza
10 Novemba 2025
Mshauri wa rais wa UAE Anwar Gargash aliyezungumza katika kongamano la kimkakati la Abu Dhabi, amesema nchi yake haijaona muundo wa wazi wa kikosi hicho cha kuleta utulivu Gaza, na katika mazingira kama hayo, huenda wasishiriki katika kikosi hicho."
Kikosi hicho kinachoratibiwa na Marekani kinatarajiwa kujumuisha wanajeshi kutoka Misri, Qatar, Uturuki, na awali UAE ilionekana kama ingeweza kushiriki.
Mnamo wiki iliyopita, Rais wa Marekani Donald Trump alieleza kuwa anatarajia kikosi hicho kufika Gaza "hivi karibuni".
Misri na Qatar zimebaki kuwa wahusika wakuu katika kuunda mustakabali wa Gaza baada ya vita.
Nchi hizo, zikishirikiana na Uturuki, zilisaini tamko la pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump, linalolenga kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yaliyofikiwa tarehe 10 Oktoba.