1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda Ukraine ikafanya uchaguzi wa rais mwezi Mei

11 Februari 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anapanga uchaguzi wa rais na kura ya maoni kuhusu amani ifikiapo Mei 15, kutokana na shinikizo la Marekani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: Alina Smutko/REUTERS

Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo na gazeti la Uingereza la Financial times. Financial Times limewanukuu maafisa wa Ukraine na nchi za Magharibi wanaolifahamu suala hilo ila hawakumnukuu Zelenskiy mwenyewe.

Kulingana na ripoti hiyo Zelenskiy anaweza kutangaza tarehe ya uchaguzi mnamo Februari 24, ambayo ni maadhimisho ya mwaka wa nne tangu Urusi ianze uvamizi wake nchini humo.

Haya yanafanyika wakati ambapo bunge la Umoja wa Ulaya leo limeidhinisha mkopo wa yuro bilioni 90 kwa ajili ya kuinusuru hali ya nchi hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha.

Chini ya mkopo huo, Ukraine itatumia yuro bilioni 60 kununua silaha za kupambana na Urusi.

Mkopo huu wa Umoja wa Ulaya unakuja wakati ambapo taasisi moja imeripoti kuwa mwaka jana, msaada wa kijeshi kwa Ukraine ulifikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kushuhudiwa, baada ya Marekani kuondoa ufadhili wake, na kuiacha Ulaya ikiwa mfadhili wa pekee.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW