1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda wavamizi wa bunge walinuia kuwateka na kuwaua wabunge

15 Januari 2021

Waendesha mashtaka nchini Marekani sasa wanasema waandamanaji waliolivamia bunge wiki iliyopita walikuwa wanataka "kuwateka na kuwauwa" wabunge.

BdTD USA | Demonstranten im Kapitol
Picha: Manuel B. Ceneta/AP/picture alliance

Waendesha mashtaka hao wameyasema hayo katika kesi ambayo walikuwa wanamtaka jaji mmoja aendelee kuwazuia Jacob Chansley kutoka Arizona na mtu aliyepigwa picha akiwa amejivalisha pembe akiwa katika afisi ya Makamu wa Rais Mike Pence katika bunge la seneti wakati wa uvamizi huo.

Mawakili wa idara ya sheria kutoka Arizona walielezea kwa kina kuhusiana na uchunguzi wa idara ya upelelezi Marekani FBI kumhusu Chansley wakisema aliwacha ujumbe kwa Pence akimwambia, ni suala la muda tu kabla haki kupatikana.

Chansley anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadae leo. Idara ya sheria Marekani imewafungulia mashtaka zaidi ya watu 80 kuhusiana na uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita.

Chanzo: afp,reuters

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW