1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hujuma za Israel huko gaza na Lebanon

Ramadhan Ali13 Julai 2006

Kuchafuka kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati na kujiuzulu jana kwa kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Jürgen Klinsmann, ndio mada kuu zilizochambuliwa katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Gazeti la OFFENBÜRGER TAGBLATT likichamgbua juu ya kuchafuko kwa hali ya mambo Mashariki ya kati laandika:

“Uvamizi wa Israel katika mwambao wa gaza na sasa nchini Lebanon,kumevuka mpaka wa azma ya kuwakomboa wanajeshi wake walionyakuliwa.

Madhumuni hasa ya serikali ya Israel ilikua kuonesha nguvu zake tena kwa kila hali.Kwa njia hii , utaratibu wa amani-lasema gazeti-hausongi mbele Mashariki ya kati.

Kuchukua msimamo mkali dhidi ya magaidi wa kipalestina ni sawa,lasema gazeti,wakati huo huo lakini, inapasa kufanya juhudi kuvisongeza kaika meza ya mazungumzo vikundi vinavyopenda amani miongoni mjwa wapalestina.

Hilo lilikua OFFENBURGER TAGEBLATT.

Ama gazeti linalochapishwa hamburg ABENDBLATT linaonesha kuelewa kwanini Israel yatumia mabavu kama ifanyavyo.Laandika:

Israel haiwezi kufanya jengine isipokua kutunisha misuli kuzuwia hujuma za wapalestina dhidi ya vijiji vya Israel na kunyakuliwa kwa wanajeshi wake.

Kuregeza kamba kwa aina yoyote na kuwaridhia watekanyara ,kutaoonekana na waarabu ni kuwa dhaifu,mbali na kutoa mualiko wa utekajinyara mwengine.

Kinyume na gazeti hilo la Hamburg, gazeti la KURIER kutoka WIESBADEN halioni kuwa Israel ina mkakati unaofahamika wazi:Laandika-

“Hata ukielewa uvamizi wa Israel katika Gaza na Lebanon,huoni matumaini makubwa ya Israel kujipatia usalama zaidi.Wanajeshi wa Israel wametumbukia tena katika matope yale yale yaliowanasa na kubidi kujikwamua kwa taababu hadi kujitoa.

Na hasa uvamizi wa Lebanon –mbali na shabaha ya kuwakomboa wanajeshi wake ambayo haina matumaini,Israel haioneshi lengo lililo wazi la kwa vitendo vyake.Nani wa kuhilikishwa huko-Hizbollah ? Jamhuri nzima ya Lebanon ambayo punde tu hivi imejikomboa kutoka makucha ya Syria ?”

Gazeti la RHEIN-ZEITUNG linalochapishwa mjini Koblenz linaitupia macho Mashariki ya kati nzima:

“wafuasi wenye siasa kali huko Mashariki ya Kati wanahisi wakati huu wana nguvu zaidi kuliko wakati wowote kabla.

Ni dhahiri-shahiri kuwa Wamarekani wamebanwa katika vita vichafu vinqavyowala pole pole .Ugomvi wa mradi wa kinuklia nchini Iran na kupata nguvu kwa wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan, hakutoi pumzi kwa vikosi vya Marekani.

Tawi lenye siasa kali la chama cha HAMAS na chama cha Hizbollah nchini Lebanon,vinajaribu kuidhofisha ngome ya Marekani-Israel.Kwa kufanya hivyo pia wanatokomeza matumaini yote ya kuleta amani-laandika Rhein-zeitung kutoka Koblenz.

Nalo gazeti la OSTSEE-ZEITUNG linazungumzia kujiuzulu jana kwa kocha wa Ujerumani Jürgen Klinsmann.Laandika,

“Sasa vishindo vya darini vimeishia sasa sakafuni.Kwani siku 3 baada ya shangwe kubwa na shamra shamra mbele ya lango la Brandenburg Tor,kocha wa taifa Klinsmann ametupa taula ringi-amesalim amri.Na hivyo amewavunja moyo mamilioni ya mashabiki wa Ujerumani na zaidi wachezaji wake.”

Likaongeza,

“Msiba huu uliolikumba dimba la Ujerumani una sababu zake:Klinsman amefuata tu tabia yake isio ya kigeugeu.Kwa njia ile ile alivyochachama mnamo miezi 24 kuijenga upya timu ya taifa, ndio kwa uzi ule ule analenga atakaokwenda m aishani mwake.Kwani, katika kipindi kifupi kama kocha wa Ujerumani, Klinsmann amefanya mengi zaidi kuliko wengi kati ya makocha waliomtangulia.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW