1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Hujuma za Urusi zaendelea kuutikisa mji wa Kharkiv

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Urusi imeendelea na mashambulizi ya ardhini dhidi ya Ukraine, katika eneo la Kharkiv, kwa kuyalenga maeneo mapya yenye vikundi vidogo, ili kujaribu kutanua wigo na kuviondoa vikosi vya Ukraine.

Ukraine | Mapigano uwanja wa vita
Ukraine inasema mapambano kwenye uwanja wa vita ni makali.Picha: Ukrinform/photonew.ukrinform.com/dpa/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa gavana wa eneo la Kharkiv upande wa Ukraine Oleh Synie-ghubov. Gavana huyo amesema "hali ni ngumu".

Wanajeshi wa urusi waliingia Ukraine karibu na mji Kharkiv, na kuanzisha mapambano mapya katika upande wa kaskazini mashariki. Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vya karibu miaka miwili sasa, vimekuwa kwa kiasi kikubwa vikifanyika katika  upande wa mashariki na kusini.

Siku ya Jumapili Urusi ilidai kuteka vijiji tisa katika mkoa wa Kharkiv na leo Jumatatu imedai kuwa wanajeshi wake wamechukua udhibiti zaidi na kusababisha hasara kwa vikosi vya ulinzi wa eneo hilo.