1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu dhidi ya Lai yakosolewa kimataifa

9 Februari 2026

Hukumu iliyotolewa Jumatatu dhidi ya aliyekuwa gwiji wa vyombo vya habari wa Hong Kong, Jimmy Lai, imezua wasiwasi kwa nchi za kigeni na makundi ya kutetea haki. Umoja wa Ulaya umetaka Lai aachiwe huru.

Hukumu dhidi ya Jimmy Lai imekosolea vikali kimataifa na miito imetolewa kutaka achiwe huru.
Hukumu dhidi ya Jimmy Lai imekosolea vikali kimataifa na miito imetolewa kutaka achiwe huru.Picha: Vincent Yu/AP Photo/picture alliance

Hukumu iliyotolewa leo dhidi ya aliyekuwa gwiji wa vyombo vya habari wa Hong Kong, Jimmy Lai, imezua wasiwasi kutoka kwa serikali za kigeni na makundi ya haki, lakini mamlaka za China na Hong Kong zimeitetea, zikisema ilionyesha moyo imara na thabiti wa utawala wa sheria.

Lai, mtetezi maarufu wa demokrasia mwenye umri wa miaka 78, alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia mnamo mwezi Desemba ya kula njama ya kushirikiana na vikosi vya kigeni na kula njama na wengine kuchapisha makala za uchochezi.

Washtakiwa wenzake, ambao walikiri kosa la mashtaka yanayohusiana na ushirikiano, walihukumiwa vifungo gerezani kati ya miaka sita na miezi mitatu, na miaka 10.

Umoja wa Ulaya na baadhi ya serikali za kigeni na makundi ya haki za binadamu yametaka kuachiliwa kwa Lai, raia wa Uingereza.

Lakini wizara ya mambo ya nje ya China imesisitiza kwamba Lai ni raia wa China, na kuzihimiza nchi nyingine kuuheshimu uhuru wake na utawala wa sheria wa Hong Kong.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW