Hukumu kutolewa dhidi ya daktari wa zamani wa Rwanda
30 Oktoba 2024Mahakama ya mjini Paris nchini Ufaransa inatarajiwa hivi leo kutangaza hukumu yake katika kesi dhidi ya daktari wa zamani wa Rwanda anayetuhumiwa kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mnamo 1994.
Wakili Mkuu anayesimamia kesi hiyo aliomba kifungo cha miaka 30 jela kwa Eugène Rwamucyo, daktari wa zamani mwenye umri wa miaka 65 anayeshtakiwa kwa mauaji ya kiholela, kushiriki uhalifu dhidi ya ubinadamu na kupanga kufanya uhalifu.
Soma pia: Wanyarwanda wakumbuka miaka 30 ya mauaji ya kimbari
Amekanusha kufanya makosa yoyote. Miongo mitatu tangu mauaji ya Rwanda, mashahidi walisafiri kwenda Paris kutoa ushahidi katika kesi iliyodumu wiki nne na kutoa maelezo ya kutisha ya mauaji katika eneo le Butare ambako Rwamucyo alikuwa wakati huo.
Hii ni kesi ya saba inayohusiana na mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 kuwahi kusikilizwa katika mahakama ya mjini Paris katika muongo mmoja uliopita.