1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Hukumu kesi dhidi ya Joseph Kabila yaahirishwa Kongo

13 Septemba 2025

Mahakama ya Kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeiahirisha hukumu juu ya kesi ya uhaini inayomkabili aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila hadi Septemba 19.

Joseph Kabila
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph KabilaPicha: Qin Lang/Photoshot/picture alliance

Mahakama hiyo ambayo iliisikiliza kesi bila Kabila kuwepo mwezi Julai, ilikubali kufungua tena kesi hiyo baada ya wito wa dakika za mwisho wa kutaka mashtaka yaainishwe kuwa ya kufanya Ujasusi. 

Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 na kuiongoza Kongo hadi 2019. Aliondoka nchini humo mwaka 2023 na alirejea mwezi Mei mwaka huu ambapo alifikia mashariki mwa Goma, eneo linalokaliwa na waasi wa M23.Bunge la Kongo lilimuondolea kinga ya mashtaka ili kuruhusu ashtakiwe. Kando ya uhaini, Kabila anashutumiwa kwa uhalifu wa kivita na kushirikiana na waasi wa waasi wa M23 ambao wanashikilia maeneo makubwa ya eneo la mashariki mwa Kongo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW