1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya wauguzi 5 Libya

20 Desemba 2006

Wahariri wa magezeti ya leo ya Ujerumani walichambua zaidi mada 2: Kwanza hukumu ya kuuliwa wabulgaria 5 na mpalestina 1 Libya na pili kustawi uchumi wa ujerumani:

Gazeti la General Anzeiger linalochapishwa mjini Bonn,likizungumzia hukumu iliopitishwa Libya laandika:

„Amri kutoka juu imetekelezwa.Kwani muda mfupi kabla ,kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi akirudia mara kwa mara tena hadharani, kuwa itolewe adhabu kali kwa wauguzi hao 5 wa kibulgaria .Azma yake ni wazi kabisa:Baada ya kulipa fidia kubwa ya fedha kwa wahanga wa ajali ya ndege ya Lockerby na hujuma katika disco ya ‚La Belle’ mjini Berlin ,akihitaji chambo kisiasa ili kuzishinikiza nchi za magharibi zinapoikaribia tena Libya.“

Gazeti la Wiesbadener Kurier likiwa na maoni sawa na hayo laandika:

„Gaddafi akiwa muungajimkono wa zamani wa ugaidi na sasa amegeuka ,anabainika kupitisha wakati katika kisa hiki.Kwa njia hiyo lakini anazichemsha nyoyo za umoja wa ulaya na serikali ya Bulgaria ambazo zilidai kunusuru maisha ya wauuguzi hao wa kibulgaria.Kwani, hapa fedha nyingi zinahusika.Fidia iliopendekezwa kwa jicho lake ni ndogo mno.Pengine,anatumai kuridhiwa mambo zaidi ya kisiasa.“ Kurier.

Ama gazeti la ALLGEMEINER ZEITUNG kutoka Mainz,linahisi msimamo wa Gaddafi umedhofika:

Linasema haifahamiki kigogo imara cha Libya kinashindwa sasa kuumaliza mkasa huu wa miaka 8 wa kuambukizwa watoto ukimwi.Badala ya ufumbuzi, wauguzi hao 5 wa kibulgaria walipitishiwa upya adhabu ya kifo kwa kuwaambukiza maradhi ya ukimwi watoto 400 wa kilibya.Hata ikiwa ni kweli wao ndio dhamana ya maumbukizo hayo, jambo ambalo ni vigumu kuamini, basi wangesathiki tu kupewa adhabu ya vifungo korokoroni na wala sio kunyongwa.

Inabainika kana kwamba, kiongozi wa Libya ambae zamani akionekana mshupavu kabisa kutokana na sababu za ndani ya Libya,hathubutu tena kusema ukweli wa mambo ulivyo-ni uchambuzi wa Allgemeine Zeitung kutoka Mainz.

Maoni ya NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld ni kuwa hukumu iliopitishwa ni ya kukasirisha mno hatan ikiwa kwa uhakika mkubwa haitatekelezwa .Yadhihirika utulivu wa ndani nchini Libya ni muhimu zaidi kwa Muamar gaddafi kuliko haki na usuh7uba mwena kambi ya magharibi.

Libya ni mojawapo ya muuzaji mkubwa mafuta na gesi kwa nchi za ulaya.Na makampuni ya magharibi yamejipanga foleni kujipatia mikataba ya kibiashara ya kujenga viwanda vya Libya .Hii haitoi matumaini mema kwa haki za binadamu- ni maoni ya NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld.

Matumaini ya kuboreka kwa hali ya uchumi wa ujerumani jinsi yalivbyo mazuri haikuwahi kuonekana tangu nchi 2 za Ujerumani kuungana.Muongozi wa IFO-INDEX umepanda licha ya mpüango wa kuongeza kodi ya mauzo kuanzia mwakani.Hii haikufumbiwa macho na wahariri wa magazeti ya Ujerumani:

Gazeti la kibiashara linalochapishwa mjini Düsseldorf-Handelsblatt laandika:

„Laiti hili lisingekua swali la matumaini tu,mtu angeweza kudai :sasa ni rasmi-uchumi wa Ujerumani utavumulia kupandishwa kwa kodi ya mauzo iliopangwa mwakani na kuendelea kustawisha uchumi.Na hilo mtu aweza kweli kutarajia kutokana na taarifa zilizotolewa hivi punde na IFO-INDEX….