1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hungary huenda ikaondoa pingamizi lake la msaada kwa Ukraine

17 Januari 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema anaamini kuwa Hungary itaondoa pingamizi lake la msaada wa dola bilioni 54 kwenda kwa Ukraine

Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Yves Herman/REUTERS

Von der Leyen ameliambia bunge la Ulaya kwamba ana imani kuwa suluhu juu ya mkwamo huo itapatikana.

Mnamo mwezi Disemba, mwaka jana Waziri Mkuu wa Hungary mwenye kuegemea siasa za mrengo wa kulia Viktor Orban, ambaye pia ni mshirika wa karibu wa Urusi, alikataa kutia saini msaada zaidi wa kifedha kwenda kwa Ukraine.

Blinken asema Marekani itaendelea kuisaidia Ukraine

Viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya walikubaliana kufanya tena mkutano mjini Brussels Februari 1 ili kujaribu kuishawishi Budapest kubadili msimamo wake, pamoja na kujadili kwa upana juu ya bajeti ya umoja huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW