1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiHungary

Hungary yataka kujiondoa kutoka sheria za uhamiaji za EU

8 Oktoba 2024

Hungary inafikiria uwezekano wa kujiondoa kutoka kwenye sheria za uhamiaji za Umoja wa Ulaya. Mahakama ya Ulaya ya Haki (ECJ) iliiamuru Hungary kulipa faini kwa kutobadilisha sera yake ya kuomba hifadhi.

Janos Boka
Waziri wa Hungary anayehusika na masuala ya Umoja wa Ulaya Janos BokaPicha: Zoltan Mathe/MTI via AP/picture alliance

Waziri wa Hungary anayehusika na masuala ya Umoja wa Ulaya Janos Boka ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kuwa, tayari amemuandikia barua Kamishna wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya Ylva Johansson kuhusu nia ya Hungary.

Katika barua hiyo, Boka ameeleza kuwa Hungary inaamini juu ya kuanzisha tena udhibiti wa mipaka yake kama sehemu ya kukabiliana na uhamiaji haramu ambao unatishia usalama wa taifa.

Soma pia:  Orban atahadharisha Ulaya, China zaelekea vita vya kiuchumi

Amefahamisha kuwa iwapo kutafanyika marekebisho ya mikataba ya Umoja wa Ulaya juu ya sheria za uhamiaji, basi Hungary itaiga mfano uliochukuliwa na Uholanzi wa kudhibiti mipaka yake.

Hata hivyo Boka amesema Hungary itaendelea kujitolea kuheshimu mikataba ya visa ya Schengen inayomruhusu mtu kusafiri ndani ya eneo la Schengen lenye mataifa 27.