1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hungary yatishia kuzuia vikwazo vipya vya EU dhidi ya Urusi

13 Mei 2023

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Hungary Péter Szijjártó ametishia kuzuia awamu mpya ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi.

Peter Szijjarto | ungarischer Außenminister
Picha: Danil Shamkin/NurPhoto/picture alliance

Ni baada ya benki kubwa ya biashara nchini Hungary, OTP kuorodheshwa kuwa miongoni mwa taasisi ambazo huenda zitalengwa na vikwazo hivyo.

Mwanadiplomasia huyo amesema iwapo benki hiyo itaendelea kuwemo kwenye orodha iliyotolewa na Ukraine ya taasisi zinazoiunga mkono Urusi, nchi yake haitaidhinisha duru mpya ya vikwazo.

Soma zaidi:Hungary yalegezewa masharti na EU iunge mkono vikwazo vya mafuta dhidi ya Urusi

Akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Umoja wa Ulaya unaofanyika nchini Sweden, Szijjártó, amesema ni jambo la kashfa kwa Ukraine kuijumuisha benki hiyo katika orodha yake wakati haijakiuka sheria yoyote.

Ukraine inaizingatia benki ya OTP kuwa taasisi yenye ushirika wa karibu na Urusi na inaituhumu kufadhili shughuli za kifedha za Moscow.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW