IAEA: Hakuna hatari Zaporizhzhia baada ya umeme kukatika
1 Oktoba 2025
Matangazo
IAEA imesema hakuna hatari katika kinu hicho kinachodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine kwa sababu jenereta za dharura zinaendelea kufanya kazi.
Shirika hilo limesema hiyo sio hali inayopaswa kuendelea kwa kuzingatia suala la usalama wa nyuklia.
Siku ya Jumanne, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya kuhusu kitisho kinachoweza kutokea akisema hali katika kinu hicho ni mbaya.
Aidha, shirika la habari la Urusi, RIA limetangaza Jumatano kuwa uongozi uliowekwa na Urusi katika kinu hicho umesema usambazaji wa umeme wa dharura unatosha.
Hata hivyo, wamesema kuanza tena usambazaji umeme kupitia njia ya Dneprovskaya, hakuwezakani kutokana na mashambulizi ya Ukraine.