1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

IAEA: Iran haiko wazi katika mpango wake wa nyuklia

14 Februari 2024

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, IAEA Rafael Grossi amesema Iran imejitenga na uwazi kuhusu mpango wake wa nyuklia,

Austria | Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, akihutubia wanahabari wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Austria, Jumatano, Novemba 22, 2023.Picha: Matthias Schrader/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, IAEA Rafael Grossi amesema Iran imejitenga na uwazi kuhusu mpango wake wa nyuklia, na hasa baada ya afisa wake aliyeongoza progamu ya  nishati hiyo wa Iran, Ali Akbar Salehi  hivi karibuni kutangaza ina uwezo wote wa uundaji wa silaha katika mamlaka yao. Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi wa serikali huko Dubai kiongozi huyo amesema hali hiyo inaongozea mkusanyiko wa mambo magumu katika eneo pana la Mashariki ya Kati wakati huu wa vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza. Baada ya kuvunjika kwa mkataba wa nyuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, inadaiwa kuanza urutubishaji wa nyuklia chini ya viwango vya kiwango cha  uundwaji wa silaha.Lakini pia imekusanya uranium iliyorutubishwa vya kutosha kuunda silaha ikiwa inataka kufanya hivyo.