1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA : Urani ya Iran inashikiliwa maeneo yanayojulikana

19 Oktoba 2025

Wakaguzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, IAEA hawaamini kuwa Iran imeficha kiasi kubwa cha urani iliyorutubishwa katika maeneo tofauti.

Austria, Vienna 2025 | Mkuu wa IAEA
Mkuu wa IAEA, Rafael GrossiPicha: Helmut Fohringer/APA/picture alliance

Kulingana na mkuu wa IAEA Rafael Grossi, taarifa zilizoko katika shirika hilo la IAEA, zinaonyesha kuwa urani hiyo kwa kiasi kikubwa imehifadhiwa katika vinu vya nyuklia vinavyojulikana huko Isfahan na Fordo, na kwa kiasi fulani huko Natanz lakini alikiri kuwa huenda kiasi kidogo pia kilipelekwa mahali pengine.

Grossi amebainisha kuwa mnamo mwezi Juni, maeneo ya nyuklia huko Isfahan, Fordo na Natanz yaliharibiwa vibaya katika mashambulizi ya Israel na Marekani.

Grossi amesema wakaguzi wa IAEA wataweza kufikia maeneo hayo wakatu tu ambapo Iran italichukulia suala hilo kuwa la kitaifa.