1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

IAEA yamezuiwa kufika maeneo ya kiwanda cha Zaporizhzhia

Josephat Charo
4 Januari 2024

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, IAEA Raphael Grossi amesema wachunguzi wake walizuiwa wasifike maeneo ya kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine kinachokaliwa na Urusi.

Mkuu wa shirika la kimaraifa la Nyuklia Rafael Grossi
Mkuu wa shirika la kimaraifa la Nyuklia Rafael GrossiPicha: Leonhard Foeger/REUTERS

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za nyuklia, IAEA Raphael Grossi amesema wachunguzi wake walizuiwa wasifike maeneo ya kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine kinachokaliwa na Urusi.

Grossi amesema wachunguzi katika kiwanda hicho hawajaruhusiwa kuingia katika kumbi mbili kubwa za mtambo wa kwanza wa pili na wa sita.

Grossi pia amesema hii ni mara ya kwanza kwa wachunguzi kuzuiwa kufika maeneo hayo na timu yake itaendelea kuomba waruhusiwe. Amesema kufikia sasa bado hawajapokea mipango ya matengenezo ya kiwanda hicho kwa mwaka huu wa 2024.