1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

IAEA yatoa onyo kuhusu kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia

6 Machi 2024

Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani IAEA Rafael Grossi, amesema leo kuwa shirika hilo limeionya Urusi dhidi ya kukifungua tena kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia Kusini Mashariki mwa Ukraine.

Mwanajeshi wa Urusi akipiga doria katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia
Mwanajeshi wa Urusi akipiga doria katika kinu cha nyuklia cha ZaporizhzhiaPicha: Andrey Borodulin/AFP

Grossi alikuwa akijibu pendekezo la shirika la usimamizi wa nyuklia la Urusi kwamba kinu hicho kianze kutumika tena.

Grossi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hatua hiyo sio ya kuchukuliwa hivi karibuni na kwamba amekuwa akiwaeleza wenzake  wa Urusi ukweli kwamba hatua yoyote kama hiyo inahitaji kuzingatia masuala kadhaa.

Kwanza kabisa, Grossi amesema kuwa eneo hilo ni uwanja wa mapigano na pili, shughuli katika kinu hicho zimesimamishwa kwa muda mrefu.

Soma pia: IAEA yamezuiwa kufika maeneo ya kiwanda cha Zaporizhzhia 

Grossi hakufutilia mbali mpango wa kufunguliwa tena kwa kinu hicho cha nyuklia katika siku za baadaye lakini amesema, kutahitajika kufanywa tathmini kadhaa za kiusalama.

Kinu cha Zaporizhzhia kilichotekwa na Urusi katika siku za mwanzo za vita vyake nchini Ukraine, kimefungwa tangu mwaka 2022 kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW