ICC kutathmini kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta
18 Machi 2013Mjini The Hague Uholanzi leo alasiri mahakama ya ICC inatarajiwa kufanya kikao maalum kilichoitishwa na majaji kutathimini athari zinazoweza kuonekana katika kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa wa kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa kenya mwaka 2007, baada ya mwendesha mashataka mkuu wa mahakama hiyo wiki iliyopita kutangaza uamuzi wa kuibwaga kesi dhidi ya mtuhumiwa mwengine katika kesi hiyo aliyekuwa mtumishi wa umma Francis Muthaura. Leo mawakili wa rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta wanategema kuitia msukumo pia mahakama hiyo kuitupilia mbali kesi dhidi ya mteja wao. Hata hivyo kumekuwa na maswali mengi juu ya jinsi mahaka hiyo inavyoiendesha kesi hiyo,hasa kutokana na suala la ushahidi katika upande wa mwendesha mashataka wa mahakama hiyo. Nimezungumza na mwanasehria wa Kimataifa kutoka London Gordon Mwikira juu ya suala hili na kwanza anatoa tathmini yake juu ya kesi hiyo ilivyo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed Khelef