Waendesha mashitaka wa ICC wanafuatilia hali ya Venezuela
12 Agosti 2024Uchaguzi huo ulimpa ushindi Rais Nicolas Maduro lakini upinzani umesema unao ushahidi unaoonesha mgombea wao wa kiti cha urais ndiye alishinda na kwamba upande wa Maduro ulitumia njia za udanganyifu.
Soma pia: Upinzani Venezuela waitisha maandamano ya dunia Agosti 17
Tangu wakati huo vikosi vya usalama vilivyo tiifu kwa Mafuro vinaendesha operesheni ya kuzima sauti za upinzani ikiwa ni pamoja na wale wanaokataa matokeo ya uchaguzi.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Karim Khan imesema imepokea ripoti kadhaa za vurugu na ukandamizaji tangu kumalizika kwa uchaguzi huo wa rais wa Julai 28.
Soma pia: Maduro akataa kukimbia Venezuela
Ofisi hiyo pia imesema imewasiliana na serikali ya Venezuela kuikumbusha umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria na kulindwa kwa haki za watu wote dhidi ya vitendo vya jinai kama ilivyoanishwa kwenye mkataba wa Roma ulioasisi mahakama ya ICC.