1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiSudan

ICC yamkuta na hatia Mkuu wa wanamgambo Janjaweed wa Sudan

6 Oktoba 2025

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumatatu imemtia hatiani mkuu wa wanamgambo wa Janjaweed wa Sudan kutokana na vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mkuu wa wanamgambo wa Sudan wa Janjaweed Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman
Mkuu wa wanamgambo wa Sudan wa Janjaweed Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, anayejulikana pia kama Ali Kushayb akisikiliza mashataka yake katika Mahakama ya ICCPicha: Koen van Weel/ANP/picture alliance

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, anayejulikana pia kama  Ali Kushayb , alipatikana na hatia ya makosa mengi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na ubakaji, mauaji na mateso yaliyotekelezwa kati ya Agosti 2003 na Aprili 2004 vilivyofanywa wakati wa mashambulizi ya kikatili huko Darfur , lakini mwenyewe alikana mashtaka hayo.

Joanna Korner, Jaji kiongozi wa ICC yenye makao yake mjini The Hague Uholanzi amesema mahakama hiyo inao ushahidi wa kutosha kuwa mshtakiwa aliyekuwa mkuu wa wanamgambo wa Janjaweed huko nchini  Sudan  ana hatia kwa makosa yanayomkabili huku akisisitiza kuwa hukumu ya adhabu yake itatolewa hapo baadaye.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW