1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yaonya dhidi vitisho kwa watendaji wake

4 Mei 2024

Waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu-ICC wametoa onyo dhidi ya "watu wanaotishia kulipiza kisasi" dhidi ya mahakama hiyo au wafanyikazi wake, wakisema kuwa vitendo kama hivyo vinaweza kuwa kosa.

Kolumbien | PK Karim Khan
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Karim KhanPicha: Chepa Beltran/LongVisual via ZUMA Press/picture alliance

 

Hata hivyo ICC haikusema kama onyo hilo linahusiana na uchunguzi wake kuhusu uhalifu wa kivita unaoweza kufanywa na Israel au makundi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinonesha kuwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ICC inaweza kutoa waranti ya kukamatwa dhidi ya wanasiasa wa Israel na viongozi wa Hamas.

Awali Ijumaa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Karim Khan, yenye makao yake makuu mjini Hague, ilisema kwenye mtandao wa X, wa zamani wa Twitter, kwamba inataka kushirikiana vyema na wadau wote kwa mazungumzo yenye kuhusu mamlaka yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW