1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

ICJ kuamua juu ya kuondoka kwa vikosi vya Israel mjini Rafah

23 Mei 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itatoa uamuzi kesho juu ya hatua zaidi za kisheria za kuzuia mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kujibu ombi la Afrika Kusini.

Wanajeshi wa Israel
Wanajeshi wa IsraelPicha: Francisco Seco/AP/picture alliance

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itatoa uamuzi kesho juu ya hatua zaidi za kisheria za kuzuia mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kujibu ombi la Afrika Kusini.

Mahakama hiyo ya ICJ, imesema leo kwamba uamuzi huo utatangazwa wakati wa kikao cha umma kwenye kasri ya Amani mjini The Hague nchini Uholanzi hapo kesho mchana. Jaji msimamizi wa mahakama ya ICJ Nawaf Salam atasoma uamuzi huo.

Soma pia:Norway, Ireland, Uhispania kutambua taifa la Palestina 

Uamuzi huo unahusu ombi la Afrika Kusini la Mei 10 mwaka huu kuhusu matumizi ya Mkataba wa Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza pamoja na ombi la dharura la Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kujiondoa kwenye mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Ingawa maamuzi ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa yanafunga kisheria, mahakama hiyo haina njia ya kulazimisha kutekelezwa kwake.

Hata hivyo, inaweza kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW