Idadi ndogo ya wapiga kura yashuhudiwa nchini Tanzania
29 Oktoba 2025
Vituo vya kupiga kura katika baadhi ya maeneo yenye shughuli nyingi zaidi jijini humo vilikuwa tupu saa moja baada ya kufunguliwa, licha ya kuwa na shughuli nyingi wakati kama huo wakati wa chaguzi zilizopita.
Haya yameripotiwa na shirika la habari la AFP.
Watu kuhamasishwa kupiga kura
Afisa mmoja kutoka chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani Temeke Dar es Salaam, aliyezungumza na AFP kwa sharti la kutotajwa jina, amesema watawahamasisha watu mitaani na majumbani kutoka na kupiga kura.
Awali shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilaani kile ilichokitaja kuwa "wimbi la ugaidi" kabla ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na "kutoweka na kuteswa kwa watu pamoja na mauaji ya kiholela ya viongozi wa upinzani na wanaharakati.