1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi Ukosefu wa kazi Ujerumani yapungua

29 Septemba 2005

Karlsruhe:

Idadi ya wasio na kazi nchini Ujerumani imepungua. Taarifa ya ofisi kuu ya kazi ya Shirikisho imesema karibu watu 79,000 wamejipatia ajira ikilinganishwa na hali ilivyokua mwezi uliopita wa Agosti. Hata hivyo taarifa hiyo imekuja katika wakati ambao kampuni la magari la ubia , la Ujerumani na Marekani DaimlerChrysler, likitangaza upunguzaji mkubwa wa wafayankazi. Idadi ya wasio na kazi hivi sasa nchini Ujerumani ni karibu milioni 4 na 650,000 .

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW