1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSri Lanka

Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Sri Lanka yakifikia 159

Saleh Mwanamilongo
30 Novemba 2025

Mamlaka nchini Sri Lanka zinapambana na mafuriko yanayoongezeka katika maeneo ya mji mkuu Colombo, baada ya Kimbunga Ditwah kuacha uharibifu mkubwa na kuua watu 159 kote nchini.

Mafuriko yakumba mji mkuu wa Sri Lanka huku idadi ya vifo kutokana na kimbunga ikifikia 159
Mafuriko yakumba mji mkuu wa Sri Lanka huku idadi ya vifo kutokana na kimbunga ikifikia 159Picha: AFP

Mamlaka nchini Sri Lanka zinapambana na mafuriko yanayoongezeka katika maeneo ya mji mkuu Colombo, baada ya Kimbunga Ditwah kuacha uharibifu mkubwa na kuua watu 159 kote nchini.

Zaidi ya watu 203 bado hawajulikani walipo, huku mvua kubwa ikisababisha maji ya Mto Kelani kufurika. Rais Anura Kumara Dissanayake ametangaza hali ya dharura na kuomba msaada wa kimataifa.

India imetuma misaada na helikopta mbili kwa operesheni za uokoaji, huku Japan ikiahidi msaada zaidi. Zaidi ya nyumba 20,000 zimeharibiwa, na watu 122,000 wamehifadhiwa kwenye kambi za muda.

Zaidi ya watu laki nane wanahitaji msaada, na karibu theluthi moja ya nchi haina umeme na maji safi. Kimbunga Ditwah kimekuwa janga baya zaidi nchini humo tangu mwaka 2017.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW