Idadi ya vifo vya mafuriko nchini Kenya yaongezeka
2 Mei 2026
Matangazo
Vifo saba vimeripotiwa mashariki mwa nchi, huku madaraja mawili yakiharibiwa katika kaunti za Kwale na Kitui. Maporomoko ya ardhi pia yameripotiwa katika kaunti ya Elgeyo Marakwet eneo la Bonde la Ufa.
Mamlaka zinasema kiwango kikubwa cha mvua na ardhi iliyojaa maji kimeongeza hatari ya mafuriko. Usafiri umeathirika baada ya baadhi ya barabara kufungwa kutokana na maporomoko ya ardhi.
Shirika la Msalaba Mwekundu linasema kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa za watu kupotea na familia kukwama katika eneo la Mukuru Kwa Njenga jijini Nairobi.