idadi Waliokufa shambulio la bunduki Urusi yapindukia 100
23 Machi 2024Mkasa huo umetokea kwenye mji mkuu, Moscow na inaelezwa kwamba washambuliaji waliingia kwenye jumba moja la starehe wakiwa wameficha nyuso zao na kuanza kufyetua ovyo risasi pamoja na kuvurumisha mabomu yaliosababisha kuzuka kwa moto.
Kundi linalojiita dola la Kiislamu IS limedai kuhusika na shambulio hilo baya zaidi kutokea nchini Urusi. Waziri wa afya Urusi Mikhail Murashko amesema watu wengine kadhaa wamelazwa hospitalini kufuatia mkasa huo, wakiwemo watoto huku mmoja kati ya hao yuko katika hali mahututi.
Soma pia:Watu 60 wauawa kufuatia shambulizi kwenye tamasha la muziki
Mamlaka nchini humo imesema uchunguzi wa "kigaidi" umeanza na rais Vladimir Putin amekuwa akipokea taarifa za kila wakati.
Tayari watu 11 ikiwemo wanne wanaoshukiwa kufanya shambulizi hilo wamekamatwa.