1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPakistan

Idadi waliouawa mashambulizi ya Pakistan yafikia 39

26 Agosti 2024

Watu 39 wameuawa katika msururu wa mashambulizi yanayowalenga maafisa wa polisi kusini magharibi mwa Pakistan, raia na wasafiri.

Pakistan | Mashambulizi dhidi ya raia na maafisa wa usalama
Athari za mashambulizi ya watu wenye silaha nchini Pakistan.Picha: Rahmat Khan/AP Photo/picture alliance

Kulingana na msemaji wa eneo hilo Shahid Rind mapema leo, magaidi walianzisha mashambulizi katika maeneo matatu tofauti yaliyolenga reli, bomba la gesi na vituo vya polisi.

Karibu watu 23 waliuawa alfajiri ya leo baada ya watu waliokuwa na silaha kuwalazimisha abiria kushuka kwenye treni na mabasi, kukagua utambulisho wao na kuwaua wote waliotokea jimbo la Punjab.

Abiria waliuliwa katika wilaya ya Musakhail, ambako washambuliaji waliweka vizuizi kwenye barabara kubwa inayokutanisha majimbo na kuchoma magari.

Watu wengine 10, polisi watano na raia watano waliuliwa kwenye wilaya ya Kalat, amesema Ihsanullah Khan, wa jeshi la polisi la eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW