1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Idadi ya vifo nchini Sudan yapindukia watu elfu 2

16 Juni 2023

Idadi ya vifo katika vita nchini Sudan yapindukia watu elfu 2

Sudan West Darfur | Geneina
Picha: Str/AFP

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limesema kuwa mapigano hayo yamesababisha watu milioni 2.2 kutoroka makazi yao, ikiwemo watu 528,000 waliokimbilia mataifa jirani. Mohamad al- Hassan Othman, mmoja kati ya mamilioni ya raia waliotoroka mapigano hayo makali katika mji mkuu Khartoum, amesema kuwa katika matarajio yao mabaya zaidi, hawakutarajia vita hivyo kuendelea kwa muda mrefu hivyo. Othman ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kila kitu maishani mwao kimebadilika na hawafahamu iwapo watarejea tena nyumbani ama watahitajika kuanza maisha mapya.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni zaidi za Mradi wa Data za Eneo la Migogoro ya Silaha zilizoorodhesha mapigano hayo hadi Juni 9, idadi ya vifo imepindukia watu hao 2,000.

Umoja wa Mataifa walaani mauanji ya gavana Abakar

Katika eneo la Magharibi la Darfur, mapigano hayo yalisababisha kifo cha gavana Abakar, saa chache baada ya kutoa matamshi ya kuwakosoa wanajeshi hao katika mahojiano ya simu na kituo cha televisheni cha Saudi Arabia.

Khamis Abdullah Abakar- Gavana aliyeuawa Darfur MagharibiPicha: SUNA/AFP

Umoja wa Mataifa umesema maelezo ya mashahidi yanahusisha kitendo hicho na wanamgambo wa Kiarabu na kikosi cha RSF huku chama ya mawakili wa Darfur kikilaani tukio hilo kilichokiita la kinyama na ukatili. Burhan ameshtumu kikosi cha RSF kwa mauaji hayo lakini RSF imekanusha kuhusika na kusema inayalaani mauaji hayo ya Abakar.

Martin Griffiths aonya kuwa hali katika eneo la Darfur yageuka kuwa janga la kibinadamu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya ubinadamu, Martin Griffiths ameonya kuwa hali katika eneo la Darfur inageuka kwa haraka kuwa janga la kibinadamu. Katika taarifa, Griffiths amesema kuwa dunia haipaswi kuacha hali hili kuendelea na kutaja hali halisi katika eneo hilo kuwa ndoto mbaya.

Marekani yalaumu jeshi la Sudan na RSF

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imelalamika kuhusu ghasia hiyo za Darfur na kuziita ukumbusho wa kutisha wa umwagikaji damu wa miaka 20 iliyopita ambao ulisababisha vifo vya maelfu ya watu. Msemaji wa wizara hiyo Matthew Miller, amesema kuwa huku maasi yanayofanyika Darfur, kimsingi yakihusishwa na RSF na wanamgambo husika,  pande zote mbili zimehusika na unyanyasaji, akimaanisha jeshi la Sudan na kikosi hicho cha wanamgambo cha RSF.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW