1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Idadi ya vifo kutokakana na mafuriko Somalia yakaribia 100

24 Novemba 2023

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyoikumba Somalia inakaribia 100, huku takriban watu milioni mbili wakiwa wameathirika.

Waokoaji wakimuokoa muhanga wa mafuriko akipelekwa na maji Somalia
Waokoaji wakimuokoa muhanga wa mafuriko akipelekwa na maji SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na Baraza la Mawaziri la nchi hiyo ambalo limesema idadi kamili sasa imefikia vifo 96. 

Mapema mwezi huu, serikali mjini Mogadishu ilitangaza hali ya dharura kutokana na mafuriko hayo yaliyopelekea takriban watu 700,000 kuyahama makazi yao huku mashamba na miundombinu kadhaa vikisombwa na maji.

Soma pia:Wasiwasi wa mafuriko watanda Sudan kufuatia shambulizi katika bwawa

Eneo la Pembe ya Afrika linakumbwa na mvua kubwa za El Nino na ambazo zinatarajiwa kudumu eneo hilo hadi angalau mwezi Aprili mwakani. 

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi huku makumi ya watu wakiwa tayari wamepoteza pia maisha katika mataifa mengine kama Kenya na Ethiopia.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW