1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 yaongezeka Italia

Zainab Aziz Mhariri:Buwayhid, Yusra
22 Machi 2020

Karibu watu 800 wamefariki katika siku moja, na kuifanya nchi hiyo kuwa ndio iliyoathirika zaidi duniani kutokana na ugonjwa COVID-19. Jumla ya watu 4,825 wameshakufa hadi sasa.

Italien - Bergamo - Coronavirus
Picha: picture-alliance/AP/C. Furlan

Katika juhudi yake ya hivi karibuni ya kukabiliana na janga la virusi vya corona vinavyosambaa na kuwaambukiza watu kwa haraka nchini humo, Italia imeamuru kufunga karibu biashara zote hadi Aprili 3, isipokuwa zile za muhimu kama zinazohusika ugavi wa mahitaji muhimu nchini kote.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema huduma hizo ni pamoja na maduka ya kuuza chakula, maduka ya kuuza dawa na huduma ya posta ni miongoni mwa huduma zitakazoendelea kufanya kazi kwa ajili ya kukimu mahitaji ya watu ya kila siku.

Idadi ya vifo ulimwenguni kote kutokana na janga la virusi vya corona imepindukia watu 11,000 huku zaidi ya watu 286,000 wakiwa wameambukizwa.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe ContePicha: AFP/D. Leal-Olivas

Takriban watu bilioni 1 kote ulimwenguni wamebaki majumbani wakati ambapo nchi kadhaa zimeweka amri ya kutotembea bila ya kuwa na sababu maalum katika harakati za kuzuia kuenea maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya COVID-19.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anaamini njia ilizotumia China kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona zinaweza kutoa mwanga wa matumaini katika kupambana na janga hili ijapokuwa wapo wanaohoji ikiwa mkakati wa China unaweza kufuatwa na nchi zingine.

Viongozi wa kidini wanaunga mkono hatua za watu kubakia majumbani mwao ili kuepusha mikusanyiko mikubwa ya watu ambapo hatari ya maambukizi inaweza kuwa kubwa.

Vyanzo:/RTRE/AFP/https://p.dw.com/p/3ZqzG

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW